Wakati timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ikicheza mechi ya kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Kenya bila ya nahodha wake Mbwana Samatta na kulazimishwa sare ya goli 1-1,Samatta allikuwa uwanjani nae akipambana kuhakikisha klabu yake ya KRC Genkinashiriki Europa League msimu wa 2016/2017.
KRC Genk imefanikiwa rasmi kupata nafasi ya kucheza Europa League msimu wa 2016/2017 baada ya kufanikiwa kuifunga Charleroi kwa jumla ya goli 5-1, Genk walianza kupata goli la uongozi kwa penati kupitia Nikolaos Karelis aliyefunga hat-trick dakika ya 20, 56 na 71 lakini Mbwana Samatta akafanikiwa kufunga goli dakika ya 27 kabla ya Sandy Walsh kufunga goli la tatu dakika ya 45.
Goli pekee la Charleroi lilifungwa na Jeremy Perbet dakika ya 40 ya mchezo, kwa matokeo hayo KRC Genk inayochezewa na mtanzania Mbwana Samatta watacheza michuano ya Europa League msimu wa 2016/2017 pamoja na vilabu vya Man United naSouthampton, hiyo itakuwa ni fursa nyingine kwa Samatta kuonekana.
KRC Genk wataanzia katika hatua ya mtoano na kama watafuzu ndio watapangwa katika hatua ya Makundi ya Europa League, makundi ambayo yatachezeshwa droo hivyo inaweza ikatokea bahati Kwa KRC Genk ya Samatta kupangwa hata na klabu kubwa kama Man United endapo itafuzu mechi yake ya mtoano
.
.
0 comments:
Post a Comment