Good news kwa watu wangu wa Bongo Flevani kwani kila mwaka wasanii wa muziki kutoka nyumbani wanazidi kuipa industry ya Entertainment nuru kubwa katika kuuwakilisha muziki wetu kwenye levo mbalimbali za kimataifa.
Wasanii wa Bongo Fleva wanaipeperusha tena bendera ya Tanzania kwani majina yao yamepata nafasi ya kuingia katika orodha ya wale wote watakaowania tuzo za KORA-Africa Music Awards kwa mwaka 2016, na watu hao ni, Vanessa Mdee, Diamond Platnumz, Yamoto Band, Wakazi na Mrisho Mpoto!
Kingine kikubwa cha kufahamu kuhusu tuzo hizi ni kwamba msanii atakaye ibuka mshindi kwenye kipengele cha Msanii Bora wa Bara (Best Artist of The Continet) atapokea zawadi ya Tsh. Bilioni 2 (dola milion 1)… na washindi watakaonyakuwa tuzo ya Best Male Artist- West Africa, Best Female Artist- West Africa, Best Male Artist East Africa, Best Female Artist East Africa, Best Male Artist- Central Africa, Best Female Artist- Central Africa, Best Male Artist-South Africa, Best Female Artist- South Africa, na Best Male Artist North Africa na Best Female Artist North Africawataondoka na zawadi ya Tsh. milion 100 kila mmoja (sawa na dola 50,000)!
Washindi wa vipengele vitakavyobakia wataondoka na zawadi yao ya Tsh Milioni 43 kila mmoja pesa ambayo kwa dola za Kimarekani ni sawa na dola 20,000.
Hii ni orodha kamili ya wale wote watakao wania tuzo za KORA- African Music Awards 2016:
Utaratibu wa jinsi ya kupiga kura bado haujawekwa wazi lakini cha kufahamu kwa sasa ni hiki, Tuzo za KORA -African Music Awards zitafanyika tarehe 20 March 2016, Namibi
a
a
0 comments:
Post a Comment