Mgombea ubunge wa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika jimbo la Tunduru Kaskazini,Mhandisi Ramo Makani alianguka jukwaani wakati akijaribu kuruka kichura chura.
Tukio hilo lilitokea katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za mgombea huyo, uliofanyika kwenye viwanja vya baraza la Idd mjini hapa.
Inasadikiwa kuwa alikusudia kunogesha staili ya mgombea urais wa tiketi ya CCM,Dr. John Magufuli ya kupiga Push Up..
Ingawa tukio hilo lilionekana kumfedhehesha,mgombea huyo alijikakamua kuinuka huku akisaidiwa na walinzi wake na kuendelea kunadai sera zake.
Alisema kuwa katika kipindi kilichopita alitekeleza ilani ya chama chake kwa kusimamia ujuenzi wa barabara ya Namtumbo-Tunduru hadi wilayani Nanyumbu inayoendelea kujengwa kwa kiwango cha lami.
0 comments:
Post a Comment