Balaa limezidi kumkumba rais wa Fifa Sepp Blatter ambaye inaarifiwa kuwa amesimamishwa kwa muda wa siku 90 kufuatia kashfa mpya ambayo imeibuka hivi karibuni ndani ya shirikisho hilo ikihusisha malipo ya fedha ambazo ziliandikishwa kwa akaunti ya rais wa shirikisho la vyama vya soka barani Ulaya Michel Platinni .
Blatter atasimamishwa rasmi baada ya kufuatwa kwa mchakato wa itifaki ambapo mwenyekiti wa kamati ya maadili mjerumani Hans Joachim Eckert anagoja kuthibitisha hatua hiyo ambayo inachukuliwa na kamati yake .
Pamoja na mambo mengine Blatter ameshutumiwa kwa kuidhinisha malipo ambayo yamefanywa na Fifa kwenye akaunti ya Platinni pamoja na kuingia mikataba kadhaa kinyume na kanuni za Fifa mikataba ambayo imehusisha makamu wa rais wa zamani Jack Warner
0 comments:
Post a Comment