Saa kadhaa baada ya shirikisho la soka Tanzania TFF kupitia kamati ya nidhamu ya TFFkutangaza kumfungia mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Haji Manara kwa utovu wa nidhamu na kukutwa na makosa matatu.
Haji amefungiwa bila kusikilizwa kutokana na kamati hiyo kutojiridhisha na dharura yake, Haji baada ya kusikia kafungia aliandika hivi kupitia instagram yake “Unazuia na kutonipa nafasi ya kusikilizwa,unanipa hukumu kwa makosa nisiondikiwa ktk mashtaka yao,,Nipo tayari kwa ajili ya mapambano, tukutane juu @simbasctanzania @tanfootball“
Haji Manara amefungiwa mwaka mmoja kujihusisha na soka pamoja na faini ya Tsh Milioni tisa, kamati ya nidhamu ya TFF imetoa adhabu hiyo licha ya Haji Manara kushindwa kufika kwa madai ya kupata dharura lakini anayo nafasi ya kukata rufaa
.
.
0 comments:
Post a Comment