Baada ya habari za mshambuliaji wa zamani wa Simba Emmanuel Okwi kuvunja mkataba na timu ya Sonderjyske Fodbold ya Denmark kwa kinachodaiwa kuwa ni kukosa nafasi ya kucheza, Haji Manara wa Simba ameuanzisha huu utani huku ikiaminika kwa sasa Okwi anarudi Simba.
Mkuu huyu wa idara ya habari na mawasiliano Simba baada ya taarifa za ujio wa Okwi Simba kuzidi kuenea, ametumia time kuendeleza utani wake kwa mahasimu wao Yanga kuwa staa huyo anakuja wasiogope na kwamba Jumapili anawasili Tanzania.
Manara amesema ‘Kocha Omog ikimpendeza Emmanuel Okwinho dimbani February 18, hiyo ndio habari mpasuko, ukinuna ongeza limao…‘
Akaendelea kwa kusema ‘Hivi nyie Ndala mbovu mnamuogopa Okwi kuliko Mungu? mngemuogopa Manani hivyo pepo mngeipata, sasa kwa taarifa yenu Jumapili tafuteni chupa msage‘
‘Habari ya Okwinho isilete mjadala town, narudia……. kocha akimpanga February 18 atacheza, Gongowazi jamaa yenu atakuja soon msiumie sana Wazee wa Fo Fo, nawatakia Jumaa Kareem’ – Manara
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Emmanuel Okwi aliuzwa na Simba kwenda kucheza soka Denmark katika klabu ya Sonderjyske Fodbold kwa mkataba wa miaka mitano na alitambulishwa rasmi na timu hiyo July 10 2015
.
.
0 comments:
Post a Comment