Ligi Kuu England inaendelea leo kwa michezo miwili kuchezwa, wakati unasubiri mchezo wa Everton dhidi ya Man United, timu ya Liverpool ikiwa ugenini katika uwanja wa Goldsands imecheza dhidi ya wenyeji wao AFC Bournemouth.
Kama ni shabiki wa Liverpool najua utakuwa umesikitishwa na goli la goli la AFC Bournemouth lililofungwa dakika ya 90 ya mchezo na kuifanya Liverpool kutoka uwanjani vichwa chini kwa kufungwa goli 4-3.
Magoli ya AFC Bournemouth yalifungwa na Callum Wilson dakika ya 56 kwa penati, Ryan Fraser dakika ya 76, Steve Cook dakika ya 79 na Nathan Ake dakika ya 90, huku Liverpool walianza kupata goli mapema tu dakika ya 20 kupitia Sadio Mane, Divock Origi dakika ya 22 na Emre Can dakika ya 64
0 comments:
Post a Comment