Staa wa soka wa kimataifa wa Ureno anayeichezea Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo amefanikiwa kushinda tuzo yake ya nne ya Ballon d’Or 2016, Ronaldo alikuwa akiwania tuzo hiyo huku mshindani wake mkuu akiwa ni Lionel Messi.
Ronaldo ameshinda tuzo hiyo kwa mara ya nne akiwa kazidiwa mara moja na Lionel Messi aliyewahi kushinda mara 5, kwa mwaka 2016 Ronaldo ameisaidia Ureno kushinda Euro 2016, lakini katika mwaka 2016 pia Ronaldo amefunga jumla ya magoli 38 katika mechi 42 na assist 14.
Staaa huyo pia amehusika katika upatikanaji wa magoli 39 ya Ligi Kuu Hispania LaLiga katika mechi 30 huku yeye akiwa kafunga magoli 31 na assist 9, tuzo hiyo imepatikana kwa mfumo wa waandishi wa habari 173 dunia nzima kupiga kura.
“Sikuwahi kufikiria akilini mwangu kama ningeweza kushinda Ballon d’Or mara nne, najivunia sana ushindi huu na nina furaha, nitumie fursa hii kuwashukuru wachezaji wenzangu wote wa timu ya taifa na Real Madrid kwa kunisaidia kushinda tuzo hii binafsi” >>> Ronaldo
0 comments:
Post a Comment