Aliyekuwa nyota wa timu ya soka ya Cameroon Samuel Eto'o huenda akahudumia kifungo cha miaka 10 jela baada ya waendesha mashtaka kumhusisha na kashfa ya kukwepa kulipa ushuru.
Huenda pia akalipa faini ya zaidi ya Euro milioni 18.
Kulingana na ripoti mchezaji huyo wa zamani wa Cameroon pamoja na mshauri wake Josep Maria Mesalles wameshtumiwa kwa kulinyima taifa la Uhispania Euro milioni 3.8 kutoka mwaka 2006 hadi 2009,wakati alipoichezea klabu hiyo ya Barcelona.
Mchezaji huyo atajiunga na Neymar na Messi,wote wakiichezea Barcelona ambao wanakabiliwa na mashtaka kama hayo.
Kashfa inayomuandamana Eto'o inashirikisha madai ya kuhamisha haki za matumizi ya picha yake katika kampuni za Uhispania na Hungary ili kukwepa kulipa kodi, katika mikataba iliodhinishwa kama vile makubaliano yake na kampuni ya jezi za michezo Puma.
Waendesha mashtaka waliwasilisha malalmishi dhidi ya mchezaji huyo ,lakini naye akatoa taarifa inayolaumu swala hilo kuwa ''uonevu na ushauri wa kifisadi''.
Eto'o ambaye kwa sasa anaichezea klabu ya Uturuki ya Club Antalayaspor,anaaminika kutolipa fedha alizodaiwa hatua ambayo imesababisha kuanzishwa kwa mashtaka hayo.
0 comments:
Post a Comment