Princes Kasune ni mmoja ya wanaharakati maarufu wa ugonjwa wa ukimwi nchini Zambia na alichaguliwa kama mbunge wa upinzani mwezi Agosti.
Aligunduliwa kuwa na virusi vya HIV mwaka 1997 na mwaka uliofuatia alitangaza hadharani hali yake kinyume na mapenzi ya mmewe na tamaduni kwa kufanya hivyo.
"Wakati niligundua kuwa nilikuwa na virusi vya HIV, nilijua kuwa nilikuwa na jukumu la kueneza habari kuhusu njia HIV unaweza kuambukizwa, unaweza kuzuiwa na pia njia za kumaliza unyanyapaa," Kasume mwenye umri wa miaka 40 aliiambia BBC.
Katika sehemu kubwa ya maisha yake, amethirika na virusi vya HIV. Alilelewa kijijini na aliwapoteza wazazi wake wote kwa ugonjwa wa ukimwi akiwa na umri wa miaka 14 na kisha akaolewa akiwa na umri wa miaka 18.
Akiwa na ndoto na kuona kizazi kichajo kisicho na virusi vya ukimwi, uamuzi wake wa kutangaza hadharani hali yake ulizua tofauti kubwa.
Kanisa lake lilimtimua kwa kuchukua hatua hiyo na kwa kwenda kinyume na matakwa ya mmewe kuhusu kuweka siri hali yake ya kuishi na virusi vya ukimwi.
Amesafiri sehemu mbali mbali za dunia na kukutana na viongozi wakiwemo marais wa zamani nchini Marekani wakiwemo Bill Clinton na George W Bush pamoja na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.
Wakati mmoja akitoa hotuba, aliwakumbusha wabunge wenzake kuhusu umuhimu wa kupimwa hali zao.
BBC
0 comments:
Post a Comment