Kazi yangu ni kuhakikisha kila siku nakuletea habari mpya na uhakika popote ulipo mtu wangu na nimekula kiapo kwako kulitekeleza hilo na leo nimeipata hii kutoka nchini Misri kuhusu Mwanamke mnene kuliko wote duniani ambaye anatajwa kufikisha uzito wa kilo 500.
Kwa mujibu wa jarida la Daily Mail, inaelezwa kuwa mwanamke huyo aitwaye Iman Ahmad Abdulati mwenye miaka 36 hajawahi kutoka ndani kwa miaka 25 na amekua akiongezeka uzito wake kwa haraka mpaka kufikia kilo 500 zinazompa shida ya kujifanyia usafi na hata kula. Ripoti ya madaktari inaonesha kuwa mwanamke huyu anasumbuliwa na maambukizi ya bakteria wanaoshambulia ukuaji wa mwili.
0 comments:
Post a Comment