Rekodi za mastaa wa muziki kutoka Afrika zinazidi kuwekwa na kuvunjwa kila siku kutokana na kazi nzuri wanazozitoa. Mtu wangu leo nimeipata rekodi hii aliyoivunja msanii Diamond Platinumz kutoka Tanzania baada ya kuachiwa tu kwa video yake ya Salome aliyomshirikisha msanii Rayvanny kutoka lebo yake ya Wasafi Classic Baby (WCB).
Najua inaweza kua sio jambo geni ukisikia wimbo wa msanii kutoka Marekani umetazamwa mara nyingi kupitia Youtube, Lakini leo hii niko na hii kutoka Tanzania mtu wangu, Diamond Platinumz amefanikiwa kuweka rekodi ya kufikisha Views zaidi ya Milioni moja na nusu kwenye mtandao wa Youtube baada ya Video ya hit single ya Salome kuwekwa ndani ya siku tano tu.
Diamond Platinumz anafuatana kwa views nyingi na wasanii mapacha kutoka kundi la PSquare na video yao ya Bank Alert iliyotazamwa zaidi ya mara milioni moja na laki moja ndani ya wiki moja tangu ilipowekwa Youtube.
Video ya PSquare inasemekana kuwa imepata views nyingi kutokana na matatizo yaliyokuwepo kati yao na kupelekea kutangaza kuwa kundi limevunjika na sababu kuwa ikitajwa kuwa kaka yao mkubwa Judees Okoye ndiye alikua chanzo cha wao kutofautiana.
Ndani ya Bank Alert wanaonekana mastaa mbalimbali kama Onyeka Onwenu, Mr Ibu, Phyno na Kcee ambao pia wamechangia kuisogeza video hiyo mpaka hapo ilipo
.
.
0 comments:
Post a Comment