Dully Sykes
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Dully Sykes amesema muziki wa singeli unatokana na muziki wa mchiriku ambao ulikuwepo hapo zamani, ambao ulikuwa ukipigwa na wakazi wa Dar es Salaam, pamoja na vanga, hivyo kuupa kibali ni muziki wa kizaramo.
"Muziki wa kisingeli ni muziki wa kizaramo, kwa sababu waimbaji wengi wa singeli ni wazaramo, wenyewe chimbuko lililotokea ni wazaramo, waluguru, wakwere, na wandengereko, ni watani, yani ndiyo hao waimbaji kabisa kabisa, singeli ile kama vanga, muziki wetu sisi wazaramo ndiyo kisingeli, hata upigaji wake na kila kitu ni vanga kabisa, hapo hapo tunarudi kwenye mchiriku, na mchiriku umezaa kisingeli", alisema Dully Sykes.
Dully aliendelea kusema kuwa hiyo ni moja ya sababu inayowafanya wasanii wa muziki wenye asili ya makabila hayo kutofeli kimuziki, kwani muziki ni jadi yao.
"Nataka tu wakubali kwamba wazaramo ndo wenye muziki, kwa sababu huyo Manfongo mwenyewe kama siyo Mdengereko basi Mluguru, kama siyo Mluguru atakuwa Mzaramo au Mkwere, huyo Sholo Mwamba ndiyo hao hao watoto wa kwetu, watoto wa kizaramo, kwa hiyo wazaramo ndiyo muziki wa kwetu, ndiyo maana watoto kama sisi tunashindwa kufeli kwenye muziki kwasababu muziki ndiyo jadi yetu", Alisema Dully Sykes
0 comments:
Post a Comment