Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amesema miongoni mwa mambo aliyojipanga kuyafanya ni pamoja na kuimarisha ulinzi katika shule zote za serikali ili kudhibiti uchomaji moto wa mabweni ya shule hizo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 19 Agosti, 2016 amemuapisha Bw. Mrisho Mashaka Gambo kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Kabla ya kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Bw. Mrisho Mashaka Gambo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.
Bwana Mrisho Mashaka Gambo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Bw. Daudi Felix Ntibenda ambaye uteuzi wake umetenguliwa.
Sherehe za kuapishwa kwake zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassani, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na Naibu waziri wa TAMISEMI Suleiman Jafo bila kusahau ndugu jamaa na marafiki.
Mara baada ya kula kiapo rasmi, Gambo ameahidi kushughulikia suala la ulinzi hususani katika shule mbalimbali kufuatia matukio ya hivi karibuni ya shule mbalimbali mkoani humo kuchomwa moto.
0 comments:
Post a Comment