Mchezaji wa zamani wa timu ya taifa ya Italia na klabu ya Inter Milan ya Italia Marco Materazzi, ameamua kuweka wazi kilichomfanya apigwe na nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Ufaransa ambaye kwa sasa ni kocha wa Real Madrid Zidane.
Vile vile amekiri kwamba tukio lile lilibadilisha kabisa mfumo wa maisha yake baada ya kuanza kufuatiliwa kwa karibu sana na vyombo vya habari.
Materazzi amesema nimeamua kutoa kitabu kinachoeleza ukweli kuhusu hilo tukio kwani sikuwahi kuongea chochote kuhusiana na tukio hilo.
“Tangu siku ile, nilianza kuombwa kufanya mahojiano na vyombo mbalimbali duniani. ” Materazzi aliongea na L’Equipe (kupitia gazeti la Marca).
“Niliamua kuchapisha kitabu juu ya tukio lile kwa sababu kila mtu alikuwa akiniuliza ni kitu gani hasa nilimwambia Zidane kiasi cha kufikia hatua ya kufanya tukio lile. Maneno hayakuwa mazuri lakini hata hivyo sikupaswa kuhukumiwa kwa namna ile. Kwenye maeneo mengi ninayoyafahamu kama Rome, Naples, Turin, Milan Paris, huwa nasikiga zaidi hata ya nilichomwambia, ” aliongeza.
“Mimi nilimzungumzia dada yake na wala sio mama yake, kama ambavyo nimesoma kwenye baadhi ya magazeti. Mama yangu alikufa nikiwa kijana mdogo sana, hivyo isingekuwa rahisi kwangu kutukana tusi hilo.”
Marco Materazzi alienda mbali zaidi na kusema kwamba haelewi kwanini stori ile ilipaishwa sana na vyombo vya habari namna ile.
“Sijui kwanini stori ile iliwekwa chumvi kiasi kile. Kitu pekee ambacho naweza kukumbuka kutoka kwenye fainali ile ni magoli yangu mawili niliyofunga najua kila mtu anauliza ni nini nilimwambia Zidane hadi akapandwa na hasira na kunipiga kichwa, ni kweli maneno yangu yalikuwa ya kijinga lakini Zidane hakustahili kureact vile”.
Angalia Video jinsi ZIDANE Alivyompiga kichwa Materaz
0 comments:
Post a Comment