Gari aina ya Kaparata lililobuniwa na kijana mtanzania kutoka Gongo la Mboto Dar es Slaam Jacob Louis Kaparata (38).
Akizungumza wakati wa maonyesho ya sabasaba jijini Dar es Salaam, Kaparata ameeleza kuwa alitumia vifaa vingi vinavyopatikana hapa nchi kuunda gari hilo na kuwa miongoni mwa vitu hivyo vingine alivitengeneza mwenyewe na vingine alichukua vya aina nyingine ya magari.
Chassis nimeitengeneza kwa kutumia square pipe, bodi nimelisuka kwa kutumia brake pipes zinazotumika kutengenezea vitanda na nikatumia mabati ya gauge 18 ambayo yanatumika kutengenezea mageti,” alisema Kaparata.
Injini, diff, gear box na matairi, vyote ni vya gari aina ya Suzuki Carry. Na nimelitengeneza kwa muda wa miezi mitatu na limenigharimu kiasi cha TZS 12,850,000.
Kijana Jacob Louis ‘Kaparata’ (38) akimwelekeza mmiliki wa blogu ya Taifa Kwanza! jinsi alivyolitengeneza gari lake la kifahari aina ya ‘Kaparata’ kwa kipindi cha miezi mitatu tu.
Jacob Louis ‘Kaparata’ akiingia kwenye gari lake alilolitengeneza mwenyewe kwa miezi mitatu.
Jacob Louis ‘Kaparata’ akiingia kwenye gari lake alilolitengeneza mwenyewe kwa miezi mitatu.
Wananchi wakipigana vikumbo kulishangaa gari la ‘Kaparata’ katika viwanja vya maonyesho ya Biashara ya Kimataifa (Saba Saba) jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa amekutana na changamoto nyingi kwenye kutengeneza gari hilo hasa suala la ufundi ambapo mara nyingine alikuwa akipeleka bati au bomba likunjwe kwa vipimo alivyotaka yeye lakini fundi anakosea hivyo inamlazimu kutupa na kuanza upya.
Changamoto nyingine ilikuwa ni kukatishwa tamaa ambapo watu walikuwa wakimwambia kuwa hawezi na kuwa suala la kutengeneza magari awaachie wazungu.
Mbali na ugunduzi huu wa kuvutia, Kaparata anafanya kazi SIDO Vingunguti ambapo anatengeneza mashine za kutotole vifaranga. Na alisema kuwa akiamua kutengeneza gari jingine, ndani ya mwezi mmoja atakuwa amekamilisha.
0 comments:
Post a Comment