Bayezid Hossain kutoka nchini Bangladesh amekuwa akisumbuliwa na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na uso wenye makunyanzi, macho yaliyotumbukia ndani, viungo vinavyomuuma, matatizo katika mfumo wa mkojo na kuwa na meno hafifu.
Licha ya kuwa anaonekana anauwezo mzuri kiakili, watu kwenye jamii wanamuogopa hata watoto wenzake hawapo tayari kucheza nae.
Mama yake amesema kuwa ameshangazwa na namna mtoto wake alivyo na uwemzo mkubwa kiakili, lakini anasikitika kwani muoneknao wake si wa kawaida. Alieleza kuwa mtoto wake huyo alinza kutembea akiwa na miaka mitatu lakini akiwa na miezi mitatu alikuwa na meno yote.
Wazazi wake wamesema kuwa mara tu alipozaliwa walishtuka kumuona kwani hata madaktari walikiri kuwa hawakuwahi kuona mtoto kama huyo.
Aidha waliporudi nyumbani, habari kuhusu mtoto huyo wa ajabu zilisambaa sana kiasi cha mamia ya watu kupanga foleni nyumbani kwao wakitaka kumuona mtoto huyo.
Rafiki pekee mtoto huyo aliyenaye ni binamu yake ambaye amekuwa akitumia muda mwingi naye. Binamu huyo hapendi kuzungumzia hali ya mtoto huyo kwani huwa inamfanya kuumia sana.
0 comments:
Post a Comment