Moroka Swallows imeinunua Free State Stars ya Bethlehem na sasa kupata haki ya kushiriki tena Ligi Kuu ya Afrika Kusini ABSA .
Mshambuliaji huyo amesema kuwa mpango wa Free State kununuliwa na Swallows umekamilika na wachezaji wote wanahamia Johannesburg leo hii.
Aidha Ngassa aliongeza kuwa wamehamia Moroka Swallows na mikataba yao inahamia kule pia, hivyo watatekelezewa haki zao kama kawaida.
Baada ya kushuka daraja kwa mara ya pili ndani ya misimu miwili, mwishoni mwa msimu wa 2015/2016, Swallows imefanikiwa kurejea Ligi Kuu kwa kuinunua Free State.
Ngassa alijiunga na Free State Stars msimu uliopita kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake Yanga na wakati anajiandaa kuingia katika msimu wake wa pili kwenye mkataba wa miaka minne timu hiyo imeuzwa
0 comments:
Post a Comment