Usiku wa July 10 2016 mchezo wa fainali ya Euro 2016 ulichezwa na kushuhudia timu ya taifa ya Ureno ikifanikiwa kutwaa Kombe la Euro kwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhid ya mwenyeji Ufaransa.
Tukio la kuumiza kwa mashabiki wa Ureno ni pale dakika ya 23 nahodha wao Cristiano Ronaldo alipotolewa nje ya uwanja kwa machela akiwa analia baada ya kushindwa kuendelea na mechi kutokana na kufanyiwa faulo mbaya.
Muda mfupi baada ya Ronaldo kutolewa analia, mama mzazi wa staa huyo Dolores Aveiro aliandika ujumbe wake kutumia account yake ya twitter unaoonesha kusikitishwa kwake kwa faulo aliyofanyiwa mwanae “Siwezi kumuangalia mwanangu akiwa katika hali hii (analia), huu mchezo ina maana kucheza mpira sio kumuumiza mpinzani”
0 comments:
Post a Comment