Taarifa iliyochukua vichwa vya habari vya magazeti ya leo June 01 2016 ni kuhusu mauaji ya watu wanane waliouawa na watu wanaodhaniwa ni majambazi katika kata ya Mzizima, tarafa ya Chumbageni jijini Tanga.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni ametembelea eneo hilo la msitu wa mapangopori ya Amboni na baadaye kuzungumza na wakuu wa vyombo vya ulinzi.
Msitu wa Mapangopori ya Amboni ndio unaodaiwa kuwa ni njia kuu ya watu wanaohofiwa ni majambazi waliofanya mauaji katika Kitongoji cha Kibatini, Kata ya Mzizima, Tarafa ya Chumbageni, Tanga.
0 comments:
Post a Comment