June 08 2016 Mahakama Kuu kanda ya Arusha ilitoa maamuzi kwa Isaac Abakukambaye alishitakiwa kwa kumtukana Rais John Magufuli kwenye ukurasa wake wa facebook ambapo mshitakiwa alitakiwa kulipa millioni 7 au kutumikia kifungo cha miaka 3 gerezani.
Baada ya kukiri kukiri kutenda kosa hilo mahakama iliamuru alipe fedha hizo kwa awamu mbili, katika awamu ya kwanza atalipa July 8 2016 sh mil 3.5 na August 8 2016 atalipa kiasi kilichobaki cha sh mil 3.5.
Leo June 17 2016 amekabidhiwa kitita cha shilingi milioni 4.5 kama sehemu ya kwenda kulipa faini mahakamani, fedha hizo zilichangwa na wanaharakati na wadau wa mitandao kupitia mratibu wa ukusanyaji wa michango hiyo kwa kanda ya kaskazini Ephata Nanyaro.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.Aliemtukana Raisi Magufuli Achangiwa fedha>>>>https://t.co/btiBGX6MH9 pic.twitter.com/iGEcwXs4pr— keneth ngamoga (@kenethngamoga) June 17, 2016
0 comments:
Post a Comment