Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo hatacheza mchezo wa Jumamosi dhidi ya Rayo Vallecano kwenye ligi kuu ya uhispania La Liga baada ya kuwa majeruhi wa msuli kwenye paja lake la kulia.
Kikosi hicho kinachonolewa na Zinedine Zidane kipo nyuma ya viongozi wa la liga kwa point moja pekee huku zikiwa zimebakia mechi nne pekee.
Madaktari wa Real Madrid pia wanaendelea kumfanyia uchunguzi Ronaldo kuona kama ataweza kukipiga dhidi ya Manchester City kwenye mkondo wa kwanza wa ligi ya mabingwa barani Ulaya itakayofanyika pale Etihad Jumanne ijayo.
Wakati huo huo Gareth Bale amerudi mazoezini baada ya kukosa mchezo wa Jumatano iliyopita waliposhinda mbao 3-0 baada ya kuwa na maumivu ya mgongo.
Mchezo ambao Real Madrid utakipiga siku ya kesho unakumbukwa vilivyo enzi za kocha Rafael Benitez ambaye aliiwezesha Madrid kushinda jumla ya mabao 10-2, huku Bale akitupia magoli manne peke yake.
0 comments:
Post a Comment