www.kenethngamoga.blogspot.com

Vurugu tupu umeya Kilombero vs D,salaam


kilombero Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali alikamatwa na kuswekwa rumande wakati akitaka kuingia kwenye ukumbi wa halmashauri kushuhudia uchaguzi wa mwenyekiti na makamu. mwenyekiti. 


Mbunge wa Kilombero, Peter Lijualikali

Mjini Kilombero, CCM ilishinda umeya kwa tofauti ya kura moja huku wabungewawili wa Chadema, Peter Lijualikali (Kilombero) akikamatwa na polisi na Devotha Minja (viti maalum) akizuiwa kuingia ukumbini. Wabunge watano wa viti maalum wa CCM walizuiwa kupiga kura.
Lijualikali alizuiwa kwa madai kuwa anatakiwa kuingia kwenye kikao cha baraza la madiwani wa Ifakara badala ya Kilombero.
Dar es Salaam. Sarakasi katika kinyang’anyiro cha umeya wa Jiji la Dar es Salaam na Halmashauri ya Kilombero, jana ziliendelea kwa staili tofauti; hali ikiwa tete jijiniwakati CCM ikishinda Kilombero ambako wabunge wawili kutoka Ukawa walishikiliwa na kuzuiwa na polisi.
Jijini Dar es Salaam, ambako uchaguzi umeshaahirishwa mara tatu, ya mwisho kwa kutumia zuio la uongo la Mahakama, hali bado ni tete kutokana na wajumbe wanne kuendelea kushikiliwa na polisi, huku nyumba ya mbunge wa Kawe, Halima Mdee ikifanyiwa upekuzi ambao chama chake cha Chadema kimesema kina wasiwasi nao.
Jijini Dar es Salaam, Kamati Kuu ya Chadema ililazimika kukutana kujadili hali ya uchaguzi wa Meya wa Jiji baada ya Mdee na madiwani watatu kulala mahabusu kuanzia juzi, huku kukiwa na taarifa kuwa wajumbe zaidi walikuwa wanatazamiwa kuitwa polisi kutoa maelezo kuhusu vurugu zilizotokea Jumapili iliyopita wakati uchaguzi huo ulipoahirishwa kwa kutumia amri ya mahakama ambayo ilikuwa imeshafutwa.
“Hii ni mikakati ya makusudi ya wenzetu wa CCM na Serikali ambao umefanyika ndani ya jiji la Dar es Salaam. Wanaogopa viongozi kutoka upinzani watakwenda kuyatibua,” alisema mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe.
“Kuna ufisadi mkubwa wa (Shirika la Usafiri Dar es Salaam) Uda, nyumba za jiji, viwanja vya jiji na kuna wizi mkubwa wa karandasi katika jiji.
“Tuna taarifa juu ya maandalizi ya kuvunja baraza la madiwani ili iundwe tume itakayoongoza jiji la Dar es Salaam. Mpaka sasa umeshafanyika mkakati wa makusudi wa kuigawa manispaa ya Ilala na Kinondoni ili kuvunja nguvu za Ukawa.”
Alisema mkakati ya polisi kuwakamata madiwani na wabunge wa Dar es Salaam ili baada ya hapo uitishwe  uchaguzi, wameshaubaini.
“Ukiitishwa uchaguzi Chadema tutawasha moto maana tumechoka siasa za kutishana,” alisema Mbowe, ambaye pia anaingia kwenye baraza la madiwani wilayani Hai kutokana na kuwa mbunge wa Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro.
Mbowe, ambaye alizungumza kabla ya kuingia katika kikao cha Kamati Kuu cha Chadema, alisema kikao hicho kitatoa  tamko lenye uamuzi mgumu kuhusu sakata la umeya wa jiji.
Kwa mujibu wa sheria zinazounda halmashauri, uchaguzi wa mameya na wenyeviti wa halmashauri unatakiwa kufanyika ndani ya siku 30 baada ya Uchaguzi Mkuu, lakini zaidi ya siku 100 baada ya uchaguzi mkuu, meya wa jiji la Dar es Salaam hajapatikana.
Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob alilieleza gazeti hili mambo matatu yanayowafanya CCM kuhakikisha wapinzani hawapati ushindi katika chaguzi hizo, hasa wa meya wa Jiji la Dar es Salaam na Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.
Jacob alisema kinachofanyika sasa ni kuvuruga chaguzi ili kuibuka vurugu na halmashauri zivunjwe na kuwakamata madiwani wa upinzani kwa madai ya kufanya vurugu, kisha chaguzi zifanyike wakati madiwani hao wakiwa rumande na kuiwezesha CCM kushinda kirahisi.
“Katika halmashauri hizi, CCM wana maslahi makubwa. Kuna mikataba hewa ambayo ilikuwa ikiwanufaisha wao, si manispaa. Wanajua tukiingia tutaweka wazi kila jambo pamoja na kufuta mikataba hiyo,” alisema Jacob.
“Hali ya mameya na wenyeviti wa halmshauri za wilaya kuwa makada wa CCM ilikinufaisha chama hicho. Sasa wanataka waendelee kushika nyadhifa hizo ili chama kiendelee kunufaika.”
Jacob alieleza sababu ya mwisho kuwa ni uoga wa Serikali inayoongozwa na CCM, kukosolewa na upinzani.
“Mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya wamekuwa wakitoa maagizo ya kisiasa na kichama kwa viongozi wa halmashauri. Wanajua chini ya Ukawa mambo hayo hayataweza kutokea hivyo ni lazima wahakikishe hatushindi,” alisema.
Akizungumzia suala hilo mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramadhani Madabida alisema: “Kama kuna ushahidi wautoe kwa sababu wamezoea kusema.”
Alisema uchaguzi wa meya wa jiji haukufanyika kutokana na zuio la mahakama baada ya watu kufungua kesi, jambo alilodai kuwa huwezi kulaumu. “Hizi dhana (za kula fedha za miradi) labda wanazo wao (wapinzani). Pengine wao ndiyo wanataka kunufaika. Nashauri tu watoe ushahidi,” alisema.
Mradi wa Uda uliwahi kuwakosanisha wabunge na madiwani wa CCM, kiasi cha meya aliyemaliza muda wake, Didas Masaburi kujikuta akiwaelezea wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam waliokuwa wakikosoa uuzwaji wa shirika hilo kuwa wanafikiri kwa kutumia makali
KUTOKA GAZETI LA MWANANCHI

i
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment