Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba Hadji Manara amesema haoni nafasi ya nyota Haruna Niyonzima kusajiliwa klabuni hapo licha ya kuwa yeye binafsi anamhusudu kwa uwezo wake.
Mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Hadji Manara akizungumza na waandishi wa habari
Akizungumza hii leo jijini Dar es salaam Manara ameyasema hayo akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya wao kama Simba watamuhitaji Niyonzima ambaye mkataba wake na klabu yake ya Yanga kuvunjika hapo jana.
Manara amesema yeye binafsi anapenda aina ya uchezaji wake uwanjani na ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa lakini haoni nafasi ya yeye kutua Msimbazi kwa kuwa dirisha la usajiri limefungwa hivi sasa .
Hata hivyo Manara amesisitiza kuwa suala la usajili lipo mkononi kwa kamati ya usajili na uongozi wa juu wa klabu hivyo yeye hana mamlaka yoyote japo kuwa hata uongozi wake unafahamu kuwa anamkubali nyota huyo
0 comments:
Post a Comment