Mgombea wa urais kupitia chama cha demokrasia na maendeleo chadema na anayeungwa mkono na vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi ukawa mh Edward ngoyai lowasa amewaahidi wakazi wa Dar es saalam kuwa kama watampa ridhaa ya kuongoza nchi atahakikisha kuwa ndani ya siku mia moja ya utawala wake anapunguza foleni pamoja na kuhakikisha madawa yanakuwepo ya kutosha kwenye hospitali.
Mh Edward lowasa ameyasema hayo katika mkutano uliohudhuliwa na mamia kwa maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es saalam kwenye viwanja vya Tanganyika pakers kawe.Mh lowasa amesema kuwa serikali yake itaweka misingi ya utawala bora kwa kujenga kituo maalum ambacho kitakuwa kinatumika na wananchi kuajili ya kupata taarifa mbalimbali toka selikalini.
Akishangliwa na mamia kwa mami ya watu waliojitokeza katika mkutano huo Mh lowasa amesema jambo kubwa ambalo linasumbua kichwa chake kwa mda mrefu ni umaskini wa watanzania ambao umesababishwa na chama kilichopo madarakani.
Mh Lowasa ambae ametumia muda mwingi kuelezea namna atakavyopambana na umaskini amesema kuwa”UMASIKINI SIO KIPAJI WALA SIO NEEMA TOKA KWA MUNGU NACHUKIA UMASIKINI AND IAM TIRED OF IT.Mwisho wa kumnukuu.
Mh lowasa anayejipambanua kwa utokomezaji wa umasikini amehoji kuwa kama uingereza wameipa elimu kipaumbele kuliko vitu vyote kwanini isiwe Tanzania? Amehoji.Hata hivyo mh lowasa ameahidi kuwa pindi selikali yake itakavoingi madarakani suala la elimu litakuwa mbele kuliko jambo lingine lolote.
Kwa upande wake naibu katibu mkuu wa chama cha Chadema bara JONH JONH MNYIKA ameionya tume ya taifa ya uchaguzi kutokufwata maelekezo ambayo yanatolewa na watawala wa Nchi huku akisisitiza kuwa mwaka huu ni mwaka wa mabadiliko na watanzania wameamua kuyafanya hivyo daftari la kupiga kura liheshimiwe.
Mnyika amewaomba watanzania kuwachagua viongozi wa ukawa kwani ndo wenye malengo thabiti ya kutatua kero zao mbalimbali.
Kwa upande wake mke wa Edward lowasa mama Regina lowasa amewaomba wakazi wa dare s saalam kutorudi nyuma maamuzi ambayo tayari wameyafanya wayatekeleze kwa vitendo siku ya kupiga kura kwa kuchagua viongozi wa ukawa katika ngazi zote za urais,ubunge,na udiwani
0 comments:
Post a Comment