Msanii wa kike anayefanya vizuri kwenye anga za muziki wa Bongo Flava Queen Darleen, amesema kitendo cha yeye kuingia Ikulu na kukaa meza moja na Rais Kikwete na kustorika nae, ni kikubwa kwake na hatokuja kusahau maishani mwake.
Queen Darleen ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema hawezi sahahu tukio hilo.
"Siku ya kwanza nilipoonana na Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, rais wetu wa Tanzania, nilipokwenda kuingia Ikulu wakati kwanza njia yenyewe kupita tu pale ni mtihani, lakini mimi niliweza kuingia kukaa kula meza moja na mama salma Kikwete na mzee mwenyewe na kupiga stori kama washkaji, kwangu ni kitendo ambacho sitakuja kukisahau katika maisha yangu mpaka nakufa", alise Queen Darleen.
Vile vile Queen Darleen amesema Rais Kikwete ndiye Rais wake wa kwanza kumpigia kura tangu azaliwe hakuwahi kupiga kura.
" Yule rais ndio rais wangu mimi kutoka moyoni na ndio alikuwa wa kwanza mimi kumpigia kura kutoka kwangu utoto mpaka kukua kwangu, siku ya kwanza napiga kura nilimpigia huyo, kwa hiyo nilikuwa natamani sana ipo siku nije kuonana nae hata kama akimaliza miaka yake nije kuonana nae, lakini kabla hajamaliza nikaonana nae akawa mshkaji wangu tunapiga stori fresh", alisema Queen Darleen.
0 comments:
Post a Comment