www.kenethngamoga.blogspot.com

Mtoto azaliwa kutoka kwa mbegu za watu watatu

Mtoto wa kwanza aliyetengezwa kwa kutumia mbinu ya uzazi wa mbegu za watu watatu amezaliwa, jarida la kisayansi la New Scientist limetangaza.

Dkt John Zhang akiwa na mtoto huyoImage copyrightNEW HOPE FERTILITY CENTRE
Image captionDkt John Zhang akiwa na mtoto huyo
Mtoto huyo wa kiume mwenye umri wa miezi mitano ana chembe chembe za DNA kutoka kwa mamake, babake pamoja na jeni za mfadhili.
Madaktari wa Marekani walichukua hatua hiyo kuhakikisha kuwa mtoto huyo wa kiume atakuwa huru kutokana na hali ya jeni ambayo mamake kutoka Jordan anabeba katika jeni zake.
Wataalam wanasema kuwa hatua hiyo ni mwamko mpya wa kimatibabu na inaweza kusaidia familia nyingine zilizo na hali za jeni zisizokuwa za kawaida.
Lakini wameonya kuwa uchunguzi wa mara kwa mara wa mbinu hiyo mpya ya kiteknolojia inayoitwa ufadhili wa Mitochondrial unahitajika.
Mitochondria ni vyumba vidogo vidogo ndani ya kila seli ambavyo hubadili chakula kuwa nguvu inayotumika mwilini.
Baadhi ya wanawake hubeba jeni zilizo na kasoro na wanaweza kupitisha jeni hizo hadi kwa watoto wao.
Wanasayansi waliohusika katika shughuli hiyo walisafiri hadi Mexico kwa sababu huko hakuna sheria za kuzuia shughuli kama hiyo ya kimatibabu.
Walichukua sehemu muhimu za chembe za kinasaba (DNA) kutoka kwa yai la mama, na DNA ya mitochondria kutoka kwa yai la mfadhili na kuunda yai lenye afya ambalo lilitungshwa mbegu kutoka kwa baba.
Matokeo yake ni kuzaliwa kwa mtoto mwenye 0.1% ya DNA kutoka kwa mfadhili na jeni nyingine zote, zinazoamua sifa kaa vile rangi ya nywele na macho kutoka kwa mama na baba.
Teknolojia mpya ya uzazi ndio iliotumika kumtengeza mtoto huyo
Image captionTeknolojia mpya ya uzazi ndio iliotumika kumtengeza mtoto huyo
Dkt John Zhang, mkurugenzi wa kimatibabu katika hospitali ya New Hope Fertility Centre jijini New York City, anasema yeye na wenzake walitumia njia hiyo kupata viinitete vitano, lakini wakastawisha kimoja tu.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment