Taarifa hii ikufikie mtu wangu wa nguvu kutoka Afrika Mashariki. Mamlaka nchini Kenya imetangaza zawadi ya dola elfu 20 za kimarekani kwa taarifa zozote zitakazosaidia kukamatwa kwa mtuhumiwa wa ugaidi anayetafutwa kwa tuhuma za kupanga shambulizi katika mji wa pwani wa Lamu.
Wizara ya mambo ya ndani ya Kenya imesema, mtuhumiwa huyo, Ramadhani Kioko, anadaiwa kuhusika na shambulizi la kigaidi lililotokea Lamu ambapo askari watano wa jeshi Kenya walijeruhiwa baada ya gari lao kukanyaga bomu lililotegwa kando ya barabara Julai 26 mwaka huu. Wizara hiyo pia imesambaza picha za mtuhumiwa huyo ambaye wanaamini kuwa alitega bomu hilo katika eneo la Ishakani, mashariki mwa mji wa Lamu.
Hatua hiyo imekuja baada ya wizara hiyo kutangaza zawadi ya dola elfu 20 za kimarekani kwa mtu yeyote mwenye taarifa zinazoweza kusaidia kukamatwa kwa mtuhumiwa mwingine wa ugaidi Abdullahi Abdi Sheikh, ambaye anadaiwa kupanga mfululizo wa mashambulizi ya kigaidi ikiwemo shambulizi lililoshindwa dhidi ya kambi ya jeshi ya Baure kwenye kaunti ya Lamu
.
.
0 comments:
Post a Comment