www.kenethngamoga.blogspot.com

UTAFITI: Watu wenye pesa nyingi waongoza kwa ulevi, Wakenya wametajwa.

Suala la unywaji wa pombe ni jambo la kawaida, lakini matumizi ya kinywaji hicho yakizidi kiwango yanaweza kukuaibisha mtu wangi. Ni kawaida pia siku hizi kupita maeneo mengi na kukuta watu wakiwa wanakunywa pombe ikiwa kama moja ya starehe muhimu kwa watu wengi

Suala la unywaji wa pombe ni jambo la kawaida, lakini matumizi ya kinywaji hicho yakizidi kiwango yanaweza kukuaibisha mtu wangi. Ni kawaida pia siku hizi kupita maeneo mengi na kukuta watu wakiwa wanakunywa pombe ikiwa kama moja ya starehe muhimu kwa watu wengi.
Nimeipata hii kutoka nchini Kenya kuhusu Utafiti uliofanywa nchini humo kuonesha kuwa, watu wenye kipato cha juu ndio hunywa pombe kwa kiasi kikubwa na kila panapokuwa na wanaume saba kwenye Bar, kuna mwanamke pia. 
Kwa mujibu wa utafiti huu uliofanywa na wizara ya afya nchini Kenya, umeongeza kuwa raia milioni 6 wa Kenya ni wanywaji waliopindukia wa vilevi.
media
Utafiti huu umeonesha kuwa, miongoni mwao watu ambao huwa wanafurahia kunywa vilevi, asilimia 24 ni watu matajiri na asilimia 18 ni watu masikini au wenye kipato cha chini, huku asilimia 50 kati yao, sio masikini wala matajiri.
Matokeo ya utafiti huu yametokana na mahojiano yaliyofanywa face to face na wahojiwa elfu 45 wenye umri wa kati ya miaka 18 na 69. Licha ya kuwa utafiti huu ulilenga kutoa mwanga kuhusu uhusiano kati ya watumiaji wa vilevi na magonjwa ya kuambukiza, umeonesha pia asilimia 13 ya Wakenya wameathiriwa na ulevi na hawawezi kuacha kunywa.
Hata hivyo asilimia ya watu wanaotumia vilevi hatari huenda ikawa ni kubwa zaidi hata kufikia asilimia 36 na idadi kubwa ya watu hawa wanapatikana kwenye maeneo ya vijijini ambako pombe hizi kupatikana kwa wingi. Utafiti huu umekuwa ni wa kwanza kufanyika nchini Kenya kuhusu magonjwa yasiyoambukiza. Daktari Gladwell Gathecha kutoka kitengo cha magonjwa yasiyoambukiza kwenye wizara ya afya, amesema kuwa, lengo lilikuwa ni kubainik hatari zinazowakabili watumiaji wa vilevi na mazingira yanayoweza kuwasababisha kupata maambukizik ya magonjwa, ili waweze kuandaa mpango wa kuzuia.
Utafiti umeonesha kuwa kwa sehemu kubwa watumiaji wa vilevi wamekuwa wakipata maambukizi yanayoweza kuepukika kutokana na kutotumia mboga za majani na matunda. Ni asilimia 6 tu ya Wakenya ndio wenye uwezo wa kupata vitamini kutoka kwenye mlo kamili, huku asilimia 94 hawana uwezo huo.
Utafiti huo pia umeongeza kuwa asilimia 84 ya Wakenya hupendelea kuongeza chumvi na Sukari nyingi wakati wa uandaaji wa chakula majumbani mwao
.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment