www.kenethngamoga.blogspot.com

Irom Sharmila: Mgomo mrefu zaidi wa njaa kumalizika

Mwanaharakati nchini India Irom Sharmila anakamilisha mgomo wake wa kukataa chakula dhidi ya sheria tata baada ya miaka 16.

Irom Sharmila
Image captionBi Sharmila amekua akipinga sheria maalum ya kiimla ya kijeshi
Mwanaharakati nchini India Irom Sharmila anakamilisha mgomo wake wa kukataa chakula dhidi ya sheria tata baada ya miaka 16.
Mwanaharakati huyo anatarajia kuanza kula hii leo baada ya mahakama katika jimbo la kaskazini mashariki mwa nchi hiyo la Manipur kumuachilia huru leo.
Amekua katika mahabusu ya mahakama na kulazimishwa kula kupitia mrija kupitia pua lake kuepuka sheria inayoadhibu uhalifu wa kutaka kujiua.
Lakini mwezi uliopita aliiambia mahakama kwamba anataka kukatiza mgomo wake na kuanza kampeni yake kama mgomea huru katika uchaguzi ujao wa wabunge .
Bi Sharmila amekua akipinga sheria inayopatia jeshi mamlaka maalum (AFSPA), ambayo inawapatia wanajeshi mamlaka yote ya kuwakamata watu bila vibali na hata kupiga risasi kwa lengo la kuua katika majimbo kadhaa nchini India , likiwemo jimbo la Manipur na la Kashmir.
Mpiga picha Ian Thomas Jansen-Lonnquist alifuatilia kwa karibu safari yake katika miaka michache iliyopita.
Irom Sharmila akiketi ndani ya chumba chake katika Taasisi ya hospitali ya chuo cha sayansi ya tiba mjini Imphal Disemba 17, 2013
Image captionIrom Sharmila
Alianza mgomo wake wa kukataa chakula miaka 16 iliyopita baada ya raia 10 kuuawa na askari wa India katika mji wa Manipur.
Ndani ya chumba cha Irom Sharmila Chanu aliwekewa mchanganyiko wa dawa uliochanganywa na maziwa ya unga ya watoto ambao alilishwa kwa mrija kwa nguvu. Mchanganyiko huo uliighalimu serikali wastani wa dola $500 kwa wiki
Image captionNdani ya chumba cha Irom Sharmila Chanu aliwekewa mchanganyiko wa dawa uliochanganywa na maziwa ya unga ya watoto ambao alilishwa kwa mrija kwa nguvu. Mchanganyiko huo uliighalimu serikali wastani wa dola $500 kwa wiki
Ameishi kipindi kirefu cha miaka 16 chini ya uangalizi wa mahakama katika hospitali ya ya mji mkuu wa jimbo la Manipur, Imphal,ambako alilazimishwa kunywa mchanganyiko wa madawa na maziwa ya unga ya watoto wachanga
Sharmila
Bi Sharmila aliachiliwa huru mwezi Agosti 2014 baada ya mahakama kukataa shitaka kwamba "anajaribu kukujiua ". Lakini alikamatwa tena siku mbili baadae baada ya kukataa kumaliza mgomo wake.
Bi Chanu akiwasili kutoka eneo alikoshikiliwa la hospitali ya taasisi ya sayansi ya tiba (JNIMS)chini ya ulinzi mkali wa polisi akielekea kwenye kesi yake iliyosikilizwa mara mbili kwa wiki katika mahakama ya juu ya Imphal, jimbo la Manipur kaskazini mashariki mwa India , kuelezea msimamo wake wa miaka 14 wakati huo wa kugoma chakula kupinga sheria inayopatia mamlaka ya ziada jeshi.
Image captionBi Chanu akiwasili kutoka eneo alikoshikiliwa la hospitali ya taasisi ya sayansi ya tiba (JNIMS)chini ya ulinzi mkali wa polisi akielekea kwenye kesi yake iliyosikilizwa mara mbili kwa wiki katika mahakama ya juu ya Imphal, jimbo la Manipur kaskazini mashariki mwa India , kuelezea msimamo wake wa miaka 14 wakati huo wa kugoma chakula kupinga sheria inayopatia mamlaka ya ziada jeshi.
Bi Sharmila alikuwa akihudhuria mahakama kuu ya Manipur kila baada ya wiki mbili kurejelea msimamo wake mgomo.
Mgomo wake wa chakula ulitambuliwa kote duniani, ambapo shirika la haki za binadamu la Amnesty International lilimuelezea kama mfungwa mwenye mawazo huru.
Waandishi wa habari wa India wakimzingira kupata maoni yake kuhusu siasa zinazoendelea kutoka Armila, 2013
Mwanaharakati huyo alivivutia vyombo vya habari vya ndani ya nchi na vya kimataifa katika miaka ya hivi karibuni .
Makumbusho ya mauaji ya Malom Massacre na kituo cha mabasi (kushoto ), vipo kwenye bara bara kuu ya kitaifa 150, na ni eneo yalipotokea mauaji ya raia 10 yaliyofanywa na wanajeshi wa India, baada ya wanajeshi kushambuliwa jana yake katika kijiji cha Malom tarehe 22.06.013.
Bi Sharmila alikua na ufuasi wa wanawake na makundi yanayopigania haki za kijamii katika jimboni.
Makumbusho ya mauaji ya Malom Massacre na kituo cha mabasi (kushoto ), vipo kwenye bara bara kuu ya kitaifa 150, na ni eneo yalipotokea mauaji ya raia 10 yaliyofanywa na wanajeshi wa India, baada ya wanajeshi kushambuliwa jana yake katika kijiji cha Malom tarehe 22.06.013.
Makumbusho yamejengwa katika eneo la Manipur ambako raia 10 waliuliwa na wanajeshi wa India. Jimbo hilo lina jumla ya wakazi milioni 2.5 na kikosi kikubwa cha wanajeshi , na polisi wengi walipelekwa huko kukabiliana na makundi ya waasi
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment