www.kenethngamoga.blogspot.com

VIDEO: Real Madrid walivyotwaa Ubingwa wa Super Cup dhidi ya Sevilla

Usiku wa August 9 2016 mchezo wa fainali ya UEFA Super Cup ulichezwa katika uwanja wa Lerkendal Norway, kwa kawaida huu ni mchezo ambao unamkutanisha Bingwa wa michuano ya klabu Bingwa Ulaya na Bingwa wa michuano ya UEFA Europa League, hivyo August 9 ilikuwa ni siku ya Real Madrid kukutana na Mabingwa wa Europa Sevilla
370D3D1700000578-3732024-The_Real_Madrid_players_celebrate_on_Rosenborg_s_Lerkendal_Stadi-a-37_1470780133796
Kwa upande wa Real Madrid wao waliingia uwanjani bila ya uwepo wa staa waoCristiano Ronaldo ambaye bado anaendelea kuuguza jeraha lake la goti, kukosekana kwa Ronaldo hakukuwa pigo sana kwani Real Madrid walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-2 ndani ya dakika 120, hiyo inatokana na dakika 90 kumalizika kwa sare 2-2.
370CB3CE00000578-3732024-Konoplyanka_who_had_a_disappointing_Euro_2016_with_Ukraine_steps-a-71_1470774989640
Mchezo haukuwa rahisi kwa Real Madrid kwani mashabiki wao walikata tamaa kutokana na mchezo hadi dakika ya 89 walikuwa nyuma kwa goli 2-1 ila dakika ya 90 Sergio Ramos akaisawazishia Real, licha ya Real Madrid kuanza kupata goli dakika ya 21 kupitia kwa Marco Asensio.
370CC3A500000578-3732024-image-a-3_1470775802102
Sevilla walifunga goli zao mbili kupitia kwa Vazquez dakika ya 41 na Konoplyankadakika ya 72 kwa mkwaju wa penati, baada ya kuongezwa dakika 30 na kuufanya mchezo kuchezwa kwa dakika 120 mechi ilizidi kuwa ngumu kwa pande zote ila Real Madridwalikuwa na bahati zaidi kuliko Sevilla kwani dakika moja kabla ya mchezo kumalizikaDaniel Ramos alipachika goli lililoipa ubingwa Real Madrid.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment