www.kenethngamoga.blogspot.com

Babu Tale asema ni bahati kwa wasanii wa ‘WCB’ kupata wanawake wenye umri mkubwa zaidi yao

Baada ya kambi ya WCB kuonekana wasanii wake wanapenda kutoka kimapenzi na wanawake wenye umri mkubwa zaidi yao, uongozi wa kambi hiyo umelizungumzia swala hilo
Akizungumza na waandishi wa habari Alhamisi hii, Mmoja kati ya viongozi wa juu wa kambi hiyo, Babu Tale, amesema ni bahati kwa wasanii wake kupata wanawake waliowazidi umri.
“Sisi tunameneji wasanii hatumeneji hisia zao, lakini ikitokea msanii fulani amempenda mwanamke fulani tunamuacha kwa sababu ni mapenzi yake,” alisema Tale. “Tunaona ni bahati kwa wasanii wetu kupata wanawake waliowazidi umri, hiyo ni bahati (anacheka) kwa sababu wanamuenzi Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alimuoa Bi Khadija ambaye alimzidi umri,”
Hata hivyo, Tale alisema ndani ya WCB hawameneji mapenzi bali wanammeneji msanii pamoja na kazi zake


VIDEO BY >BONGO5
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment