www.kenethngamoga.blogspot.com

Muhammad Ali Bondia nguli wa Marekani afariki dunia akiwa na miaka 74

Bingwa wa zamani wa ndondi na mwanaharakati wa nchini Marekani, Muhammad Ali ‘The Greatest’ amefariki dunia.
image
Ali alifariki Ijumaa hii kwenye hospitali ya huko Phoenix ambako alikuwa akitibiwa kutokana na matatizo ya kupumua.
Alikuwa na umri wa miaka 74.
“After a 32-year battle with Parkinson’s disease, Muhammad
Ali has passed away at the age of 74. The three-time World
Heavyweight Champion boxer died this evening,” Bob
Gunnell, msemaji wa familia aliiambia NBC News.
Taratibu za mazishi zinafanyika kwenye mji wake wa Louisville, Kentucky.
Bondia huyo alizaliwa kwa jina la Cassius Marcellus Clay Jan. 17, 1942 huko Louisville, Kentucky. Alianza kucheza ndondi akiwa na miaka 12 na kushinda mikanda kadhaa kabla ya mwaka 1960 kushiriki mashindano ya Olympic mjini Rome, na kushinda medali ya dhahabu. Muda mfupi baadaye aliingia kwenye ndondi za kulipwa.
Akiwa amekuwa maarufu Ali alianza kupambana na ubaguzi wa rangi nchini Marekani. Baada ya kukataliwa kupewa huduma kwenye duka la soda, alisema aliitupa medali yake ya dhahabu ya Olympic mtoni.
image
Akiwa na miaka 22, alilikataa jina la Cassius Clay kwa kudai ni la kitumwa na kuanza kujiita Muhammad Ali. Mwaka 1967, wakati wa vita vya vietnam alikataa kulitumikia jeshi la Marekani kwa madai kuwa vita hivyo havikuendana na msimamo wa dini yake.
image
Kutokana na uamuzi huo, alinyang’anywa mkanda wake na kuhukumiwa kifungo cha miaka mitano jela. Aliachiwa  baada ya kukata rufaa lakini akazuiwa kupigana au kuondoka nchini.
Baada ya kupewa tena kibali cha kupigana alimshinda Jerry Quarry na miezi sita baadaye kwenye pambano lililopewa jina ‘pambano la karne’ na kuchukua round 15, Ali alishindwa kwa mara ya kwanza na Joe Frazier.
Ali na Frazier walipigana tena mwaka 1974. Ali alishinda.
Alikuja kuuchukua mkanda wa ubingwa wa dunia kwa kumpiga George Foreman baadaye mwaka huo kwenye pambano lililopewa jina “The Rumble in the Jungle,” na kufanyika Zaire.
image
Ali alikuja kupigana tena na Frazier mara ya tatu katika pambano la mwaka 1975, “Thrilla in Manila” ambalo hadi sasa linaaminika kuwa pambano bora zaidi katika muda wote.
image
Ali aliendelea kuutetea mkanda wake hadi mwaka 1978, alipopigwa na Leon Spinks, na kisha kuuchukua tena.
Alistaafu mwaka 1979, alipokuwa na miaka 37 lakini akarudi tena mwaka 1980 na kupambana na Larry Holmes na kushindwa. Ali alishindwa tena na Trevor Berbick, mwaka uliofuata na ndipo alipoamua kustaafu kimoja.
Bondia huyo alifunga ndoa mara tatu na zote zikavunjika huku akipata watoto tisa akiwemo Laila, aliyekuja kuwa bondia pia.
image
Ali alimuoa mke wake wa mwisho, Yolanda “Lonnie” Williams mwaka 1986; na wameishi kwa muda mrefu huko Berrien Springs, Michigan, kisha kuhamia Arizona.
Bonyeza Play kuikiliza Historia ya Mohamed Ali

Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment