Robo fainali ya tatu ya michuano ya AFCON 2017 imechezwa jioni ya January 29 Gabon ikizikutanisha timu za taifa za Ghana dhidi ya timu ya taifa ya DR Congo, huo ni mchezo ambao umemamlizika kwa timu ya taifa ya Ghana kupata ushindi wa goli 2-1
.
Ushindi wa Ghana umepatika kwa Jordan Ayew kufunga goli la kwanza dakika ya 63 lakini dakika ya 79 kaka yake Andrew Ayew akapachika goli la ushindi kwa Ghana kupitia mkwaju wa penati, hiyo ni baada ya DR Congo kusawazisha goli la kwanza dakika ya 68 kupitia kwa Paul M’poku.
Kwa matokeo hayo Ghana sasa watacheza mchezo wao wa nusu fainali ya michuano ya AFCON 2017 dhidi ya timu ya taifa ya Burkinafaso ambayo jana January 28 iliifunga Tunisia goli 2-0 na kuiondoa katika michuano ya AFCON 2017.
0 comments:
Post a Comment