Watu 24 wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari mawili ya City Boy eneo la Maweni mkoani Singida
Watu 24 wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari mawili ya City Boy eneo la Maweni mkoani Singida.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamishna Msaidizi wa Polisi mkoa wa Singida Thobias Sedoyeka amesema ajali hiyo imehusisha basi lenye usajili wa no T 531 BCE likitokea Dar es Salaam kwenda Kahama na basi namba T 247 lililokuwa likitokea Kahama kwenda Dar es Salaam.
Aidha metaja mabasi hayo ni mali ya kampuni ya City Boys ambapo yamegongana uso kwa uso na kuua abiria 24 papo hapo na wengine sita kufariki baadaye na wengine kujeruhiwa na kueleza kuwa idadi ya majeruhi na vifo vitaendelea kutolewa.
0 comments:
Post a Comment