Hatimae usiku wa July 3 2016 michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya 2016 hatua ya robo fainali ilimalizika rasmi kwa robo fainali ya mwisho kupigwa katika uwanja wa Stade de France ukizikutanisha mwenyeji wa michuano hiyo kwa mwaka 2016 timu ya taifa yaUfaransa dhidi ya timu ya taifa ya Iceland.
Katika mchezo huo uliotazamiwa kupata mashabiki zaidi ya 60000, ulimalizika kwa timu ya taifa ya Ufaransa kuondoka na ushindi mnono wa magoli 5-2, magoli ya Ufaransayalifungwa na Oliver Giroud dakika ya 13 na 59, Paul Pogba dakika ya 20, Dimitri Payet dakika ya 43 na Antoine Griezmann dakika ya 45.
Wakati timu ya taifa ya Iceland ilifanikiwa kuondoka na magoli mawili pekee yaliofungwa na Kolbeinn Sigporsson dakika ya 56 na Birkir Bjarnason dakika ya 84. Kwa matokeo hayo sasa ni rasmi timu ya taifa ya Ufaransa itacheza dhidi ya timu ya taifa ya Ujerumanikatika mchezo wa nusu fainali ya Euro 2016
0 comments:
Post a Comment