www.kenethngamoga.blogspot.com

SABABU TANO KUU ZINAZOCHANGIA WASANII WENGI KUTUMIA MADAWA YA KULEVYA.

Tatizo la matumizi ya madawa ya kulevya kwa wasani hasa wanamuziki sio jambo geni masikioni mwetu,sio Tanzania tu tatizo hili lipo kwani hata katika nchi za magharibi walipojaa mastaa wakubwa wa muziki pia kuna tatizo  la matumizi ya madawa ya kulevya kwa wasanii,list ni ndefu ila badhii ya mastaa

Tatizo la matumizi ya madawa ya kulevya kwa wasani hasa wanamuziki sio jambo geni masikioni mwetu,sio Tanzania tu tatizo hili lipo kwani hata katika nchi za magharibi walipojaa mastaa wakubwa wa muziki pia kuna tatizo  la matumizi ya madawa ya kulevya kwa wasanii,list ni ndefu ila badhii ya mastaa wakubwa duniani waliowahi kukiri kujihusisha na madawa ya kulevya ni pamoja na rapper Eminem,DMX,bondia Mike Tyson,the former NBA star Lamar Odom na wengine kibao.
Kwa hapa nyumbani wapo baadhi ya wasanii waliowahi kukiri kujihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya ,miongoni mwao ni pamoja na the late pontetial rapper Langa(R.I.P),Ray C,Q-Chief, na Chid Benz,inawezekana wapo wasanii wengi wanaojihusisha na matumizi ya madawa ya kulevya ila hawajawa tayari kukiri hadharani kwa sababu zao binafsi,hivyo basi kwa kutokana na uzito wa tatizo hili,serikali,wadau wa sanaa na muziki,vyombo vya habari,mashabiki na wasanii kwa ujumla hawana budi kushirikiana katika kuepusha madhara makubwa zaidi hasa kwa wasanii wetu ambao tunaamini kupitia kazi zao wao ni kioo cha jamii.
Zipo sababu nyingi zinazopelekea wasanii kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya,ila kwa kuzingatia tafiti mbalimbali na simulizi za baadhi za wasanii walioathirika na tatizo hili la matumizi ya madawa ya kulevya,hizi ndizo sababu kuu tano za wasanii wengi nchini kujiingiza kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya.
1.KUIGA.
Baadhi ya wasanii hasa wanamuziki wamekua wakiongozwa na hisia za wasanii wenzao waliowahamasisha wao kuingia kwenye muziki,wasanii wengi nchini wamekua wakiiga mambo mengi kutoka kwa wanamuziki wa nchi za magharibi hasa marekani,badhii ya mambo hayo ni pamoja na mahadhi ya muziki,mavazi na hata mitindo ya maisha,ni wazi kuwa kuiga huku kusikozingatia hasara na faida kumepelekea wasanii wengi kujikuta wakiiga baadhi ya mambo yasiyo na faida katika maisha yao kama matumizi ya madawa ya kulevya.
Chidi benz                                                                            Chid Benz.
2.UKOSEFU WA ELIMU.
Ukosefu wa elimu,ikiwemo elimu ya sanaa ni miongoni mwa mambo yanayopelekea wasanii wengi kujiingiza katika wimbi la matumizi ya madawa ya kulevya,kwa msanii mwenye malengo na mipango ya kufika mbali kisanaa kamwe hawezi kujihusishwa na mambo yatakayoathiri sanaa yake au kumharibia sifa mbele ya jamii,msanii mwenye kuziingatia kigezo hiki cha elimu anaweza kujifunza kupitia wale walioathirika na matumizi ya madawa ya kulevya,kusikiliza ushauri kutoka kwa wadau wa sanaa na watu wanaomzunguka ili ajijenge na kuikuza sanaa yake.
DIOF                                                                      Msafiri Diof.
3.TAMAA YA FEDHA.
Wasanii wengi wamekua na tamaa ya kupata mafanikio ya muda mfupi,kila msanii ana ndoto za kujulikana na kupata umaarufu,kumiliki mali kama nyumba,magari na vitu vingine vya thamani,tamaa ya fedha imekua chachu kwa baaadhi ya wasanii wengi kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya,baadhi ya wafanyabiashara wa madawa ya kulevya wamekua wakitumia mwanya huo kwa kuwatumia wasanii kusafirisha madawa hayo,hali inayopelekea wengi wao kujikuta wakiingia katika matumizi ya madawa ya kulevya.
rayc67                                                                                      Ray C.
4.KUJIINGIZA KATIKA MAKUNDI YASIYO NA TIJA.
Katika miaka ya hivi karibuni,tumeshuhudia mabadiliko makubwa katika tasnia ya sanaa na burudani,kumekuwepo na makundi au timu miongoni mwa wasanii,wadau na hata mashabiki,makundi haya au timu hizi zimekua zikitoa support kwa kazi za wasanii wanaofungana nao,kwa wasanii ambao wamekua wakijiingiza katika makundi au timu hizi na baadae kutokea migogoro baina yao,wamejikuta wakiporomoka kisanii,kiuchumi na mwisho kujikuta wakijiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya.

chila                                                                        Q-Chief.
5.MSONGO WA MAWAZO.
Mihemko ya kihisia katika kupata mafanikio kwa baadhi ya wasanii huwasababishia msongo wa mawazo,hatuna budi kufahamu kuwa wasanii nao ni binadamu hivyo mbali na shughuli zao za sanaa,kama waalivyo watu wengine wamekua wakikabiliana na changamoto mbalimbali za kimaisha kama migogoro ya kimapenzi,kudhulumiana na watu wanaofanya nao kazi hasa za sanaa,magojwa,matatizo ya kiuchumi,na hata uadui miongoni mwao.Baadhi ya wasanii wasioweza kukabiliana vyema na changamoto hizi na nyingine nyingi,wamejikuta wakiishi katika msongo wa mawazo unaopelekea wengi wao kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya.
#SembeNoma #UsifateMkumbo
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment