www.kenethngamoga.blogspot.com

Mahali ilipo na muonekano wake wa sasa bastola ya dhahabu ya Muammar Gaddafi

Ni miaka minne imepita toka auwawe aliyekuwa Rais wa Libya kanali Muammar Gaddafi na vikundi vya waasi wa nchi hiyo, Gaddafi alikuwa 

Ni miaka minne imepita toka auwawe aliyekuwa Rais wa Libya kanali Muammar Gaddafi na vikundi vya waasi wa nchi hiyo, Gaddafi alikuwa kiongozi ambaye ana miliki vitu vya thamani kubwa kama gari la kifahari lakini alikuwa ana miliki Bastola iliyopambwa kwa dhahabu.
160203092653_gaddafi_pistol_libya_512x288_afp
Bastola ya Gaddafi baada ya kuuwawa kwake ndio ilitumika kama ishara ya ushindi kwa waasi, ambao kwa kiasi kikubwa walikuwa wanatumia kuonesha hadharani kama furaha ya ushindi wa kumuondoa Rais huyo madarakani, muandishi wa BBC Gabriel Gatehouse ambaye alikuwepo wakati wa mapinduzi ya Gaddafi, amerudi Libya kwenda kufanya stori kuhusu bastola ya dhahabu ya Gaddafi ilipo na kuhusu maisha ya waasi waliomuua Gaddafi.
150728151102_gaddafi_640x360_bbc_nocredit
Gaddafi aliuawa tarehe 20 Oktoba 2011
Mjini Misrata, kilomita 200 mashariki mwa mji mkuu wa Tripoli, ndipo inapoaminika kuwa bastola hiyo ipo kwa sasa. Mohamed ndio aliokota bunduki hiyo karibu na mahali ambapoGaddafi alikamatwa, na katika mtafaruku uliokuwepo, na pia alipoonekana na bastola hiyo, waasi wengine walidhani Mohammed ndiye aliyemuua Gaddafi, na papo hapo ndio akawa anatajwa kama shujaa wa mapinduzi nchini Libya
.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment