Bado masaa kadhaa yamesalia kuweza kushuhudia ule mchezo wa kihistoria unaozikutanisha timu kongwe Tanzania za Simba dhidi ya Yanga. September 26 ni siku ambayo klabu za Simba na Yanga zitacheza mechi yao ya kwanza ya Ligi Kuu Tanzaniabara kwa msimu wa 2015/2016, mechi ambayo itachezwa uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.
Hii ni taarifa kutoka kwa shirikisho la soka Tanzania TFF kuhusiana na mchezo huo ambao unatazamiwa kuwa na idadi kubwa ya mashabiki kuliko mechi nyingine yoyote ya Ligi Kuu Tanzania, hivyo hivi ni vitu vya kuzingatia kuelekea mchezo huo hususani katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu. Msemaji wa shirikisho hilo Baraka Kizugutoana haya kwa mashabiki watakaokwenda kutazama mechi hiyo.
“Cha kwanza tunaomba wapenzi na mashabiki wakanunue tiketi katika vituo husika kuepuka kuuziwa tiketi feki, la pili tunaomba wapenzi wanaokuja kutazama mechi hiyo kutovaa mavazi ambayo yanakuwa na mahusiano au ushabiki wowote wa vyama vya siasa, hivyo tunaomba waje wakiwa wamevaa sare za mchezo husika au timu nyingine yoyote ila sio sare za vyama vya siasa”>>> Kizuguto
0 comments:
Post a Comment