Ni Moja ya Habari zilizogusa Vichwa vingi vya Habari Duniani September 24 2015
imeripotiwa Taarifa kuhusu watu zaidi ya 700 kufariki kwenye Msikiti Mkuu ambao Waumini
wa Dini ya Kiislamu huenda kwa ajili ya Hijjah ambao uko Mecca, Saudi Arabia
Ni Moja ya Habari zilizogusa Vichwa vingi vya Habari Duniani September 24 2015 imeripotiwa Taarifa kuhusu watu zaidi ya 700 kufariki kwenye Msikiti Mkuu ambao Waumini wa Dini ya Kiislamu huenda kwa ajili ya Hijjah ambao uko Mecca, Saudi Arabia.
Sasa moja kati ya watu mashuhuda waliokuwa katika msongamano huo mkubwa uliopelekea vifo vya watu zaidi ya 700…‘Nilikuwa nimeondoka hapa majira ya saa tano asubuhi nikienda kutekeleza nguzo ya kupiga mawe nguzo moja tu ya kwanza ngumo ya Jamarati na siku ile tulikuwa tumejiandaa kwenda kupiga mawe saba kwenye nguzo moja tu, ile siku kwanza tulivyotoka kwenye kambi yetu ya zamzam zamzam ilituambia kwamba tuwe tunaotoka mmoja mmoja walisema ni vyema tusubiriane watupeleke kwa pamoja kwa utaratibu walioupanga – Shuhuda
‘Lakini sisi wengine tuliona ni vyema ngoja tuanze kwenda tulipopiga hatua ya kwanza na ya pili tukakuta barabara zimefungwa na hizo njia zilizofungwa ndio zikasababisha msongamano mkubwa wa watu ndio kupelekea kukanyangana na kuwepo kwa joto kubwa kusababisha vifo‘ – Shuhuda
‘Joto la Mecca kwa kweli hauwezi ukafananisha na sehemu yoyote hakuna hata sisi tunaoishi Tanzania ndio watu wa kwanza kuweza kuliona joto hilo kwa hiyo kulikuwa na makundi mawili ambayo yote yalikuwa yanatumia njia moja na kupelekea watu kutostahimili na kukosa pumzi katika msongamano huo ‘ – Shuhud
a
a
0 comments:
Post a Comment