www.kenethngamoga.blogspot.com

Mambo matano ya kufahamu kabla ya KRC Genk ya Samatta kucheza vs Celta Vigo leo

Usiku wa leo April 13 2017 mtanzania
Mbwana Samatta ataandika historia mpya katika maisha yake ya soka kwa kucheza game yake ya kwanza ya robo fainali ya UEFA Europa League akiwa na
KRC Genk kwa mara ya kwanza katika maisha yake

Mbwana Samatta

KRC Genk wanacheza dhidi ya Celta Vigo leo saa 22:05 kwa saa za Afrika Mashariki, Genk ya Samatta itakuwa Hispania kucheza dhidi ya Celta Vigo katika game hiyo ya robo fainali itakayochezwa katika uwanja wa
Balaidos , kuelekea game hiyo mtu wangu naomba nikupe dondoo muhimu za Celta vs Genk.
Ratiba ya mechi za robo fainali ya kwanza ya UEFA Europa League zinazochezwa usiku wa leo April 13 2017.

Mbwana Samatta anatajwa kama mchezaji wa kuchungwa katika game hiyo, kutokana na takwimu zake za kucheza mechi 6 za Genk zilizopita za mashindano yote na kufunga magoli sita ni wastani wa kufunga goli moja kila mechi.

KRC Genk wanaingia kucheza mchezo dhidi ya Celta Vigo wakiwa wanarekodi ya kucheza mechi zao sita za hivi karibuni na kutoruhusu kupoteza mchezo wowote, katika mechi sita Genk wameshinda mechi 5 na kutoa sare mechi moja.

Katika mechi tano zilizopita za mashindano yote KRC Genk wamefanikiwa kushinda mechi nne na kutoka sare mechi moja wakati Celta Vigo wameshinda mechi zao tatu na kufungwa mechi mbili.

Katika mechi 5 za karibuni Celta Vigo wamefunga jumla ya magoli 8 na kuruhusu magoli 6 wakati KRC Genk wao wamefunga jumla ya magoli 15 na kuruhusu kufungwa magoli matatu.
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa KRC Genk kucheza dhidi ya Celta Vigo katika mashindano yanayoandaliwa na UEFA.

Samatta hadi sasa amecheza jumla ya game kumi za UEFA Europa League kuanzia hatua ya makundi, akifunga magoli mawili na kutoa assist moja na hajaoneshwa kadi yoyote ile.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment