www.kenethngamoga.blogspot.com

Taarifa kuhusu stori za nyasi bandia za Simba kupigwa mnada na TRA

Moja kati ya stori kubwa iliyokuwa ikijadiliwa kwa wapenda soka bongo leo ni kuhusiana na habari za nyasi bandia za timu ya Simba kuandikwa kuwa zitapigwa mnada na mamlaka ya mapato
Tanzania (TRA) kutokana na kushindwa kuzilipia kodi bandarini, Simba waliomba msamaha wa kodi lakini imeshindikana.


Lakini kuna taarifa pia zilizotolewa baadae kuwa mtanzania Mbwana Samatta aliyewahi kucheza Simba ambaye kwa sasa anaichezea KRC Genk ya Ubelgiji amezilipia kodi hizo, ukweli kutoka katika ukurasa rasmi wa msemaji wa Simba Haji Manara na TRA ni kuwa
Samatta hajalipia kodi ya nyasi hizo.
Ukweli wa taarifa rasmi ni kuwa Simba wameongezewa muda wa siku 14 wazilipie kodi nyasi zao hizo bandia ambazo wanampango wa kuziweka katika uwanja wao wa mazoezi wa
Bunju , katika siku 14 walizopewa Simba tayari zimebakia siku tatu pekee.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment