Pichani ni mwanamke aliefanyiwa vitendo vya ukatili na mume wake huku sababu ikitajwa kuwa mwanamke huyo alipekua simu ya mumewe ndo sababu iliyomfanya mwanaume kumtoboa jicho moja
Hayo yamebainishwa na Malisa G kupitia mtandao wake wa Facebook ambapo ameonyeshwa kusikitishwa kwake na kitendo alichofanyiwa huyu mwanamke
Taarifa niliyopewa ni kwamba huyu dada anaitwa Emma Sillah. Amefanyiwa ukatili wa kiwango cha kutisha kwa kutobolewa jicho lake moja na mtu anayedaiwa kuwa mumewe wa ndoa.
Sababu ya kufanyiwa unyama huo ni baada ya kutaka kushika simu ya mumewe. Yani mke alipata mashaka na simu ya mumewe akataka kuichukua ili kuona mume anawasiliana na nani. Matokeo yake akapigwa hadi kutobolewa jicho. Inshort amekua chongo.
Kuanzia sasa hatakua na uwezo tena wa kuona kwa macho yake mawili. Atabaki mlemavu wa macho akiona kwa jicho moja hadi siku anaingia kaburini. Ukatili huu usivumiliwe. Huyu mwanaume ni muuaji. Nashauri ashtakiwe kwa jaribio la kuua (attempt to murder) na sio kosa la kujeruhi. Mtu anayekupiga kiasi cha kukupasua jicho amedhamiria kukuua sio kukujeruhi.
Lakini najiuliza, hivi mkeo unawezaje kumtenda ukatili wa kiwango hiki? Mkeo wa ndoa uliyeapa kumlinda na kumpenda unawezaje kumfanyia hivi?? No, no plz.!
Bila shaka huyu dada anaikumbuka siku ya ndoa yake na huyu mumewe aliyemgeuza mlemavu wa kudumu. Anakumbuka huyu mwanaume alipoahidi kumtunza na kumpenda maisha yake yote. Anakumbuka huyu mwanaume alipokiri kwamba yeye ni ubavu wake na atamlinda kwa gharama yoyote.
Lakini yote hayo leo yamebadilika. Mume ameona simu ya "laki 3" ina thamani kuliko jicho la mkewe. Ameamua kumteketeza mkewe ili kulinda simu yake. Upuuzi wa kiwango cha PhD. Kama hakutaka mkewe apekue simu yake si bora angeipiga hiyo simu chini ipasuke kuliko kunyofoa jicho la mkewe.!
Inaumiza sana, inasikitisha sana, inakera sana. Imagine watoto wanakua wanamuona mama yao ni chongo halafu wanamuuliza mama what happened, mama anajibu "baba yenu alinitoboa jicho ili kunizuia nisipekue simu yake" Daaah. Unadhani watoto watajisikiaje??
Anyway, nisiseme sana lakini huu ni mwendelezo wa matukio ya ukatilii wa kijinsia wanaofanyiwa zaidi wanawake nchini. Kuna baadhi ya wanaume huwaona wanawake kama vile si watu. Kama mtu anaona simu yake ina thamani kuliko uhai wa mkewe, anaweza kuthamini watu wengine kweli?
Watu kama hawa wanastahili kifungo cha maisha jela au kunyongwa hadi kufa ili iwe fundisho kwa wanaume wengine wenye ukatili wa aina hii. Lakini bado unajiuliza watoto wao wataishije? Hata akifungwa bado amemuachia mkewe mzigo mkubwa sana wa malezi.
Baba anaozea jela na mama ameshakua chongo ameachiwa watoto awalee peke yake. Anahangaikia mahitaji ya watoto kwa jicho lake moja. Daah. Huu mtihani ni mgumu sana.!
Halafu nimeambiwa huyu dada ni mjamzito. Sasa imagine anakuja kujifungua mtoto hamjui baba, maana atakua anatumikia kifungo gerezani. Mtoto anauliza, then mama anamwambia "baba yako yupo jela, wakati nikiwa na mimba yako alinitoboa jicho kunizuia nisishike simu yake". Aisee. Hili ni jaribu kubwa sana. Mungu pekee amtie nguvu huyu dada.
Halafu imagine huyu dada alivyokua anampenda mumewe kwenye simu yake alimuweka as a "profile picture" whatsapp, na akaandika maneno mazuri kuwa anamtakia heri katika siku yake ya kuzaliwa. What a great love.! Lakini jamaa limeshindwa hata kuappreciate upendo wa mkewe limekuja kumnyofoa jicho.
Nashauri vyombo vya dola vichukue hatua kali kwa huyu mwanaume. Pia nawashauri dada zangu mnapochumbiwa angalieni na aina ya wanaume wanaowachumbia. Biblia inasema "zipimeni kwanza hizo roho". Kuna wengine wana miili anadamu lakini roho za shetani.
Pole sana dada uliyepatwa mkasa huu. Najua wakati mgumu unaopitia. Mungu pekee akupiganie. Im pissed off. Nimeumia sn kwa ajili yako.!
0 comments:
Post a Comment