Ude Ude enzi za uhai wake
Kwa mujibu wa gazeti la Mwananchi wawili hao walikuwa miongoni mwa majambazi wanne waliokuwa na gari aina ya Toyota Probox waliokurupushwa na polisi katika jaribio la kuiba vifaa vya magari ya halmashauri.
Tukio hilo lilitokea jana saa mbili asubuhi walipokutwa wakivunja gari la mwalimu wa shule ya sekondari, Maweni aliyejulikana kwa jina la Dominica Tarimo.
Wananchi wakiwa na piki piki na magari pia waliungana na polisi kuwafukuza watu hao na kuwashambulia.
Polisi hao wamedai watu hao walijihami na silaha zenye ncha kali ili kujiokoa na wawili kupiga risasi huku wawili wakitokomea kwenye msitu ulio jirani na kiwanda cha saruji cha Sungura.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Tanga, Leonard Paul amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Marehemu Ude Ude wa kushoto na rafiki yake Iku ambao wote wamefariki kwenye tukio hilo
Iqu Junior amewahi kumshirikisha Alikiba kwenye wimbo wake ‘Nisamehe.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
0 comments:
Post a Comment