www.kenethngamoga.blogspot.com

Mfalme wa Japan aonyesha nia ya kuondoka madarakani, katoa sababu zake

Mtu wangu taarifa inayogonga vichwa vya habari kwa sasa kwenye vyombo vya habari vya kimataifa ni hii ya Mfalme wa Japan kuonyesha nia ya kutaka kuondoka madarakani wakati katika sheria za nchi hiyo hakuna nafasi inayomruhusu mfalme kuondoka madarakani
Mtu wangu taarifa inayogonga vichwa vya habari kwa sasa kwenye vyombo vya habari vya kimataifa ni hii ya Mfalme wa Japan kuonyesha nia ya kutaka kuondoka madarakani wakati katika sheria za nchi hiyo hakuna nafasi inayomruhusu mfalme kuondoka madarakani. 
Mfalme wa Japan Akihito amelihutubia taifa hilo kupitia runinga ambapo ameeleza kuwa ametaka kung’atuka kutokana na kwamba ana wasiwasi na umri na udhoofu wa afya yake huenda vikamfanya ashindwe kutekeleza majukumu yake.
japan 5
Wananchi wa Japan wakifuatilia hotuba ya mfalme
Lakini muda mfupi baada ya hotuba yake, Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, amesema atatathmini kwa makini nia hiyo ya mfalme huyo. Mfalme Akihito amekuwa madarakani tangu kifo cha babake, Hirohito, mwaka 1989, habari kwamba anataka kung’atuka zilianza kutokea kwenye vyombo vya habari mwezi jana.
wananchi japan
Wananchi wakionekana kushangaa baada ya Mfalme Akihito kutangaza nia yake ya kung’atuka
BBC
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment