Basi la kipekee lenye urefu wa mita mbili juu linaloruhusu magari ya kibinafsi kupitia mvunguni mwake limefanyiwa majaribio katika mji wa Hebei kaskazini mwa Uchina. Dhumuni kubwa la kutengeneza basi la aina hiyo ni  kutatua kabisa tatizo la usafiri kwa watu katika miji yenye idadi kubwa ya wakazi.
Basi hilo linaloendeshwa kwa umeme linauwezo wa kubeba zaidi ya watu 300, lina urefu wa mita 21 na upana wa futi 25 na linauwezo wa kukimbia kwa kasi ya Kilomita 60 kwa kila saa. Hii ni mara ya kwanza kwa wabunifu kuonesha basi hilo hadharani baada ya video yake kuvuja katika mitandao mwezi Mei.
Abiria wakijaribu kuabiri basi hilo la kipekee katika kituo maalum cha kuabiri mabasi hayo mjini Qinhuangdao
Maelfu ya wachina walipigwa na butwaa basi la kipekee linaloendeshwa na umeme lilipofanyiwa majaribio katika mji wa Qinhuangdao, Kaskazini mwa mwa China
Basi la kipekee la Transit Elevated Bus TEB-1 likiwa barabarani mjini Qinhuangdao, China
Abiria katika mji wa Qinhuangdao, ulioko jimbo la Hebei China wakifurahia usafiri wa siku za usoni wa Transit Elevated Bus TEB-1
Muonekano wa ndani ya basi hilo ambalo linanafasi kubwa mno ya kuweza hata kubeba abiria 300.