www.kenethngamoga.blogspot.com

BIBI WA MIAKA 60 ACHAPWA VIBOKO MBELE YA UMATI WA WATU KWA KOSA LA KUUZA POMBE

Bibi mmoja wa dini ya kikiristo amechapwa viboko mia huko nchini Indonesia ambayo hujulikana sana duniani kwa kuwa na waislamu wengi sana. Bibi huyo alikutwa na hatia ya kuuza pombe na hivyo kuamuliwa kuchapwa vikobo 30 mbele ya watu walikusanyika kushuhudia adhabu hiyo iliyotokea huko jimbo la Aceh.

aceh-woman-caned-620x378

Aceh ni jimbo pekee linalofuata sharia hiyo ya kiislamu ya kuchapa viboko hadharani endapo mtu amekutwa na makossa mbalimbali. Moja ya kosa linalo adhibiwa kwa viboko ni Uzinzi ambako waliohusika wote wanapata adhabu ya viboko 100 kwa wakati mmoja. Vile vile, adhabu hiyo hutolewa sana sana kwa wapenzi wa njiasia moja, walevi, na hata wale wanaozungumza na watu ambao hawajaoa wala kuolewa.
Adhabu hii imezoeleka kwani imeanza kutolewa tangu mwaka 2001 na kwa sasa imestaajabisha watu kwani ni mara ya kwanza kutolewa kwa mtu asiye muislamu na wakati ilikubalika kutolewa kwa waislamu pekee.
Picha za watu wakichapwa viboko kwa makosa mbali mbali:-

Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment