www.kenethngamoga.blogspot.com

Obama amuidhinisha Clinton kuwania urais Marekani

Rais wa Marekani Barack Obama ametangaza kumuunga mkono Hillary Clinton kuwa mgombea urais wa chama cha Democratic katika uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu nchini Marekani.ObamaImage copyrightGETTY
Image captionObama ataanza kufanya kampeni na Clinton
Rais wa Marekani Barack Obama ametangaza kumuunga mkono Hillary Clinton kuwa mgombea urais wa chama cha Democratic katika uchaguzi mkuu utakaofanyika baadaye mwaka huu nchini Marekani.
Amechukua hatua hiyo muda mfupi baada ya kukutana na seneta wa Vermont Bernie Sanders ambaye amekuwa akikabiliana na Bi Clinton katika kinyang’anyiro cha kumchagua mgombea wa chama hicho.
Akizungumza kwenye video ambayo imepakiwa kwenye Twitter na Bi Clinton, Bw Obama amesema mgombea huyo ndiye aliyewahi kuhitimu zaidi kuwa rais wa Marekani.
“Niko pamoja naye, nina msisimko na nasubiri sana kutoka huko nje na kufanya kampeni na Hillary,” amesema Obama.
ObamaImage copyrightREUTERS
Image captionObama alikutana na Sanders ikulu ya White House
Wawili hao sasa wanatarajiwa kuanza kufanya kampeni pamoja.
Bw Sanders naye amesema yuko tayari kufanya kazi na mpinzani wake, Bi Clinton, kumshinda mgombea wa chama cha Republican Donald Trump katika uchaguzi mkuu.
Hata hivyo hakujiondoa kinyang’anyironi. Alisema ataendelea kufanya kampeni yake na kwamba anatumai atakutana na Bi Clinton hivi karibuni.
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment