www.kenethngamoga.blogspot.com

Nukuu ya Maalim Seif ‘Lipumba asahau uenyekiti CUF’ yatolewa ufafanuzi

June 15 2016 chama cha wananchi CUF kupitia kwa kupitia kwa mkurugenzi wa habari na uenezi, Salim Bimani amekanusha taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari ambapo taarifa hiyo imesema kwamba Taarifa hii ni uongo na katibu hajaitoaa

Baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii June 15 2016  vimeamka na habari yenye kichwa cha habari ambacho kimenukuu Katibu Mkuu wa chama cha CUF, Maalim Seif akisema ‘Prof. Lipumba asahau uenyekiti CUF’.
June 15 2016 chama cha wananchi CUF kupitia kwa kupitia kwa mkurugenzi wa habari na uenezi, Salim Bimani amekanusha taarifa zilizoripotiwa na vyombo vya habari ambapo taarifa hiyo imesema kwamba Taarifa hii ni uongo na katibu hajaitoaa. Hii ni miongoni mwa propaganda zinazotengenezwa na watu wasio na malengo mema na chama, wakijua fika kwamba maamuzi ya chama hayafanywi na mtu bali vikao vya chama.
Taarifa imeongeza kuwa maoni na msimamo wa Katibu mkuu Maalim Seif ambaye yuko Marekani ni kwamba wanachama wanasubiri maamuzi ya vikao vya chama vitaamua mambo mbalimbali yanayoendelea na yanayotokea na vitatangaza maamuzi yake kwa wote.
Chama hicho kimetoa Rai kwa wanahabari kuwa makini sana na vyanzo vya taarifa mbalimbali wanavyotumia kupata taarifa hasa mitandao ya kijamii pia wafuate maadili ya uandishi wa habari na kuandika habari kutoka kwenye vyanzo vya uhakika visivyo na shaka.
Aidha CUF imetoa angalizo kwa wanachama wake wote kuwa makini na taarifa wanazopokea na wazithibitishe kwa umakini ili kuwa na uhakika na kuepuka kupotoshwa

Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment