www.kenethngamoga.blogspot.com

Mahakama yaamuru Tigo kuwalipa AY na FA shilingi bilioni 2 baada ya kutumia nyimbo zao bila ridhaa

Mahakama ya Hakimu Mkazi Ilala jijini Dar es Salaam, imeiamuru kampuni ya mawasiliano ya TIGO kuwalipa wasanii Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ na Ambwene Yessayah ‘AY’ jumla ya shilingi bilioni 2.18 baada ya kutumia kazi zao za muziki bila ridhaa yao.
 Hukumu hiyo imetolewa kutokana na kampuni hiyo kutumia kazi za wasanii hao ‘Dakika Moja’ na ‘Usije Mjini’ kama miito ya simu bila makubaliano yoyote. Hiyo inakuwa hukumu kubwa zaidi kuwahi kutolewa kwenye historia ya mambo ya ukiukwaji wa haki miliki za kazi za ubunifu na sanaa nchini.

Hakimu mkazi wa mahakama ya Ilala, Juma Hassan alitoa hukumu hiyo Jumatano hii kufuatia mvutano mahakamani kati ya pande hizo mbili uliodumu kwa kipindi cha miaka minne. Pia Tigo imetakiwa kulipa shilingi milioni 25 nyingine kama sehemu ya fidia.
Taarifa za kesi hiyo zimefahamika wiki hii baada ya wakili wa mastaa hao Alberto Msando kupost kwenye Instagram picha akiwa nao kwenye mahakama kuu jijini Dar es Salaam.

“At the High Court of Tanzania, Dar Es Salaam. #UsijeMjini #DakikaMoja #Tigo #CopyrightsInfringement #stoppingwizi @aytanzania @mwanafa,” aliandika.
Kampuni hiyo ilikuwa imepeleka pingamizi la hukumu hiyo ya mahamaka ya hakimu mkazi Ilala katika mahakama kuu ya Tanzania. Rufaa hiyo ilipangwa kusikilizwa Jumanne hii lakini imeahirishwa hadi Ijumaa.
Madai ya Mwana FA na AY ni kuwa Tigo ilitumia kazi zao bila kuwa na mkataba nao wowote au kampuni ya kati iliyowawakilisha na hivyo kuingiza fedha ambayo wawili hao wanaamini ni nyingi.
Awali walitaka walipwe fidia ya shilingi bilioni 4.3.

Chanzo: The Citizen
Ungana na mimi kupitia Facebook , Twitter na Instagram Pia subscribe Youtube ili uwe wa kwanza kupata habari mpya.
Share on Google Plus

Keneth Ngamoga

Keneth Ngamoga ni mtangazaji wa radio Pambazuko iliyopo Ifakara.Huwa akisikika katika vipindi tofauti vya burudani.Kwa msaada na ushauri Wasiliana na Keneth Ngamoga Kupitia namba
+255655632798
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment